JIFUNZE KUNYAMAZA!


USIZUNGUMZIE pesa zako mbele ya fukara na masikini.

Usizungumzie ubora wa Afya yako mbele ya mgonjwa anayeteseka na magonjwa.

Usizungumzie nguvu zako mbele ya Mnyonge tena ambaye unajua huna lengo la kumsaidia au pengine nguvu zako ndio sababu ya mateso yake.

Usizungumzie furaha yako mbele ya mwenye huzuni, vilio na majonzi.

Usizungumzie Uhuru wako mbele ya mfungwa.

Usizungumzie Mtoto/watoto wako mbele ya aliye tasa au mgumba au aliyefiwa na watoto wake.

Usizungumzie habari za wazazi wako mbele ya walio mayatima.

Usizungumzie vyakula na Vinywaji vyako mbele ya wanaolala na kushinda njaa.

Usiwazidishie maumivu, maumivu unayowazidishia yaweza kukugharimu hata wewe.

Nisikilize, iko hivi;

Umepata kazi jifunze kunyamaza!

Umepata mchumba jifunze kunyamaza!

Umepata mtoto jifunze kunyamza!

Umepitia hali ngumu kiafya, kiuchumu au kimahusiano. Hebu nyamaza kimya!

Umepata mafanikio ya kiuchumu au kimahusiano, hebu jifunze kunyamaza!

Umenunua kiwanja, umenunua gari au nyumba kaa kimya.

Mwanao amefaulu au wewe umefaulu kaa kimya.

Umevishwa pete ya uchumba/umeoa/umeolewa, hebu jifunze kunyamaza!

Mahusiano yako yameyumba, yamevunjika, mchumba kakukimbia? Ndoa iko arijojo inataka kuvunjika. Ndoa imevunjika? Nyamaza kimya!

Unajiuliza Kwa nini unyamze??

Wapo wengi wasiopenda maendeleo yako! Wapo wengi wanatumia muda wao mwingi kukiharibu kile ulichokipata! Kutangaza hatua ulizozipiga au changamoto unazopitia ni kuwapa taarifa muhimu kuwa wao waanzie wapi kuviharibu zaidi. Kaa kimya fanya mambo yako kwani siku zote Action speak louder than your words. Wacha maendeleo na changamoto zako vizungumze. Never allow your enemies to trace your next move!

Roho za binadamu zinapotoa maneno huwa yanajenga, kubomoa na hata kuumba kwa kuwa tunaamini kuwa Mungu alituumba kwa sura na mfano wake na kumbuka Mungu aliumba kwa mdomo hivyo basi midomo huumba maana ndani yetu imo pumzi ambayo ni Roho ya Mungu.

Roho za wanadamu nyingi hazipendi wewe uendelee, hazipendi wewe uwazidi sasa iweje changamoto au maendeleo kidogo tu tayari umekimbilia kuwatangazia kila kona ikiwemo Facebook, Instagram, Twitter, Telegram, Tango n.k.

Unadhani wanafurahia sana maendeleo yako? Unadhani hata ukielezea shida na changamoto za ndoa na mahusiano yako mitandaoni watakuonea huruma na kukushauri lililo jema zaidi ya kuchochea MOTO?

0 Response to "JIFUNZE KUNYAMAZA!"

Post a Comment